Nawezaje kuzuia utasa

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ikiwa haujashika mimba, usitie shaka: Wanandoa wengi hushika mimba katika mwaka wa kwanza, ikiwa watashiriki ngono wakati ambao ni rahisi kwake kushika mimba.

Epukana na hewa, chakula au maji yaliyochafuliwa na madawa ya kuuwa wadudu au kemikali zilizo na sumu ambazo hutumika mashambani na viwandani: Madawa ya kuuwa wadudu na kemikali zingine hatari zinaweza kuumiza mbegu za mwanamume anapofanya kazi. Mwanamke anapofua nguo za mume wake, kemikali hizi pia humfikia.

Usivute sigara, kutafuna tumbaku, kunywa pombe au kahawa: Wanawake ambao huvuta au kutafuna tumbaku, au wale ambao hunywa pombe au kahawa kwa wingi huchukua muda kushika mimba, au mimba zao huharibika. Wanaume ambao huvuta sigara, kunywa pombe au kahawa kwa wingi hutengeneza mbegu chache, na wakati mwingi hizi huwa zimeharibika au ni hafifu.

Tahadhari na mahali palipo na joto jingi: Mbegu za mwanaume zinahitaji mahali pasipo na joto jingi. Hii ndio sababu korodani zake zinaning'inia ndani ya scrotum, nje ya mwili wake. Korodani zinapopata joto sana, zinaweza kuwacha kutengeneza mbegu nzuri. Kwa mfano, hii inaweza kufanyika mwanaume anapovalia nguo zilizomshika mwili na kuzifinya korodani zake, au akioga kwa maji moto, au akifanya kazi karibu na majiko yenye moto mkali, tanuru, au injini haswa kwa madereva wa malori - haswa ikiwa ataendesha gari kwa muda mrefu bila ya kupumzika. Korodani zinaporudi hali yake ya kawaida, zinaanza kutengeneza mbegu nzuri.

Usitumie dawa zozote: Baadhi ya madawa yanaweza kusababisha utasa. Chaguo bora la wewe na mpenzi wako ni kutotumia dawa zozote wakati mnajaribu kushika mimba. Ikiwa ni lazima dawa itumike kwa sababu ya ugonjwa, zungumza na mhudumu wa afya na umweleze kuwa unajaribu kushika mimba.

Jaribu kushiriki ngono wakati ambapo ni rahisi kushika mimba: Ingawa mwanaume hutengeneza mamilioni ya mbegu kila siku, mwanamke hutoa yai moja pekee kila mwezi. Huu ndio wakati mzuri kwake kujaribu kushika mimba - wakati mmoja katika mwezi, ambapo anaweza kushika mimba. Kwa baadhi ya wanawake, wakati huu huanza siku 10 baada ya siku yake ya kwanza ya hedhi, ambayo huwa ni siku 6. Mwili una ishara nyingi za kukuambia kuwa ni wakati mzuri wa kujaribu kushika mimba. Ishara rahisi ya kuangalia ni mabadiliko katika kamasi ambalo hutoka kwenye sehemu yako ya uzazi.

Unaposhiriki ngono: Njia nzuri ya kuhakikisha mbegu imeingia karibu na tumbo la uzazi ni:

  • ukilala chali na mume wako akulalie juu
  • ukilalia upande wa kushoto au kulia. Baada ya ngono, lala chali kwa muda wa dakika 20. Hii itasaidia mbegu kupiga mbizi hadi kwenye tumbo la uzazi na kukutana na yai.

Usitumie mafuta wala krimu wakati wa ngono: Vitu hivi vinaweza kuzuia mbegu kufikia yai.

Usioshe ndani ya sehemu yako ya uzazi kwa maji: Ukijiosha kwa maji kabla au baada ya ngono hubadilisha unyevu ndani ya sehemu yako ya uzazi, na hii hufanya vigumu kwa mbegu kustahimili.

Pata matibabu kwa shida yoyote ya afya: Ni jambo muhimu kwako wewe na mpenzi wako kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa magonjwa ya zinaa na magonjwa mengine. Ikiwa mmoja wenu anaugua ugonjwa wa zinaa, lazima nyote mtibiwe. Hakikisha kuwa mnamaliza dawa zote mnazopatiwa.

Kula chakula kilicho na afya: Ikiwa hedhi yako haiji kwa majira na wewe ni mnene sana au mwenye mwili mdogo, jaribu kupunguza uzani au kuongeza uzani.

Usivute sigara wala kutafuna tumbaku, kutumia mihadarati au kunywa pombe.

Tahadhari sana na vinywaji kama vile kahawa, chai ya rangi (sturungi), na soda kama coca cola.

Fanya mazoezi na upumzike vya kutosha.

Muone mhudumu wa afya ikiwa baada ya mwaka mmoja hutakuwa umeshika mimba: Kuna uchunguzi fulani ambao gharama yake ni ndogo, na ambao utakueleza shida ni nini. Kwa mfano, mhudumu wa afya ataangalia mbegu za mume wako kwa kutumia kurunzi kuona ikiwa zina afya. Atakufanyia uchunguzi kuhakikisha kuwa sehemu yako ya uzazi, tumbo la uzazi na mirija haina maambukizi au vimelea. Anaweza pia kukufunza jinsi ya kutambua wakati ovari zako zinatoa yai kwa kuchukua joto lako kila asubuhi. Ni jambo la muhimu kukumbuka kuwa uchunguzi huu hukuambia tu shida iko wapi - na wala sio kuisuluhisha. Hata madawa ghali na upasuaji hauwezi kutibu utasa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011205