Ninawezaje kudumisha afya njema wakati wa ujauzito

From Audiopedia
Revision as of 17:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Unapojihudumia vyema wakati w ujauzito, waweza kuwa na mimba salama na kuzaa mtoto mwenye afya njema

Jaribu kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha. Lishe bora inakupa nguvu, yazuia maambukizi, hujenga mtoto mwenye afya, na husaidia kuzuia kutokwa na damu nyingi mno wakati wa kujifungua. Kumbuka kwamba wewe unajilisha pamoja na mtoto wako. Tumia chumvi yenye madini joto ili mtoto wako asikabiliwe na akili yenye kasi ya chini.

Lala na kupumzika zaidi. Kama wewe wafanya kazi yakusimama, jaribu kukaa au kulala mara kadhaa wakati wa mchana. Fanya kazi yako lakini jaribu kupumzika wakati wowote unaoweza.

Nenda kuona daktari kabla ya kujifungua (kabla ya kuzaa) ili kuhakikisha hakuna matatizo, na kutambua matatizo kabla yawe mabaya. Kama hujawahi kupata chanjo ya pepopunda, pata moja haraka kama unaweza. Pata angalau mara mbili kabla ya mwisho wa ujauzito.

Soma kuhusu 'Dalili za hatari wakati wa ujauzito' kujifunza wakati huu ni muhimu pia kumuona mhudumu wa afya.

Usafi muhimu. Kuoga au kufua mara kwa mara na kusafisha meno yako kila siku.

Fanya mazoezi, ndiposa uke wako uwe na nguvu wakati wa ujauzito na baada ya kuzaa.

Fanya mazoezi kila siku. Kama wewe hukaa chini kazini, jaribu kutembea kidogo kila siku. Usijichoshe na mazoezi.

Pata matibabu ikiwa unadhania kuwa uko na maambukizi ya zinaa (STI) au maambukizi mengine.

Pimwa Virusi vya ukimwi. Zuia maambukizi ya Virusi vya ukimwi wakati wa ujauzito kwa kutumia mpira wakati wa kujamiiana.

Epuka kutumia madawa ya kisasa au mitishamba, isipokuwa wakati mfanyakazi wa afya ambaye anajua wewe ni mjamzito amesema ni sawa.

Usikunywe pombe au kuvuta sigara au kutafuna miraa wakati wa ujauzito. Hizi zote ni mbaya kwa mama na zinaweza kudhuru afya ya mtoto.

Ikiwa kuna malaria mahali unapoishi, lala kwenye wavu au neti ili kuepuka kung'atwa na mbu.

Epuka dawa za kuua wadudu, au kemikali za viwanda. Zote zaweza kudhuru mtoto wako tumboni. Usifanye kazi karibu na viwanda, au kupumua katika mafusho yao. Usihifadhi chakula au maji katika vyombo vyao.

Kaa mbali na mtoto aliye na upele mwilini. Inaweza kuwa imesababishwa na German Measles, ambayo yaweza kudhuru mtoto wako.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010705