Nawezaje kuishi na migogoro ya majukumu katika ndoa

From Audiopedia
Revision as of 17:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Katika nchi nyingi, wanaume wako na mamlaka kwa hiyo kupata usaidizi wao ni muhimu. Ikiwa unataka kutafuta kazi au ungelipenda kuanzisha biashara yako, kupata usaidizi kutoka kwa mume wako kutasaidia mno.

Ikiwa unafikiria kuwa mume wako hatakubaliana na mipango yako, jaribu kutumia mbinu zifuatazo;-

1. Kabla ya kuzungumza na mumeo, fikiria vyema kuhusu mipango yako. Ikiwa hujui nini haswa unachotaka, na vile utakavyofanya, ni vipi basi anavyotarajiwa kuelewa mipango yako na kukusaidia?

2. Fanya msimamo dhabiti, lakini si kugombana, jadili mipango yako na mume, utafaulu ikiwa utakuwa mtulivu na kuzungumza naye kama rafiki yake, sio kumkaripia au kulia.

3. Tekeleza mipango yako huku ukishauriana na mumeo. Ukimuuliza akupe ushauri na mawaidha hatakuwa na wasawasi au kukushuku na kile utakachokifanya na kutambua kuwa mtafaidika na jitahada zenu.

4. Mueleze mumeo kuwa maisha yenu yatakuwa mazuri ikiwa atakusaidia kwa sababu mapato ya familia yenu yataongezeka na utatumia pesa hizo kujenga familia yenu.

5. Mwambie mumeo kuwa atakuwa kichwa wa familia tajiri na kwamba hadhi yenu itainuka katika jamii utakapoanza kupata pesa. Wanaume wengine huogopa kuwa watadharauliwa ikiwa sio yeye pekee katika familia anayepata mapato. Muelezee kuwa hii haina ukweli wa kutosha na kuwa katika visa vingi, waume wa wake wanaofanya kazi hupata heshima zaidi.

6. Pendekeza kwa mume wako kuwa mapato yako yatawasaidia kuwapa masomo mazuri watoto wenu. Kila baba hujali maisha ya baadaye ya watoto wake na hutambua kwamba katika ulimwengu wa sasa elimu ni ufunguo wa maisha na kazi ya mapato bora. Ikiwa mume anawatakia mema watoto wenu hatakataa nafasi hiyo.

7. Muonyeshe ukitumia mifano ya -- wanawake walioenda kazini au walioanzisha biashara zao vile familia zao zilivyofaidika.

8. Ikiwa baada ya kujaribu njia hizi zote, bado mumeo hakubaliani na wewe, jaribu kutafuta wahusika wengine katika familia yenu kuwasaidia kutatua shida hii. Unaweza kukutana na wanawake wengine kupata usaidizi wao na kujua jinsi walivyoweza kubadilisha mawazo ya waume wao.

MUHIMU: Usiwe na maswali mengi kuhusu mamlaka ya waume au usawa wa kijinsia kwa ujumla. Mume wako hastahili kutishiwa na mabadiliko unayoyataka.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021006