Nafaa kujua nini kuhusu dawa zilizochanganywa vidonge vya kupanga uzazi vilivyo na estrogen na progestin

From Audiopedia
Revision as of 16:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Dawa za kupanga uzazi zitakukinga dhidi ya kupata mimba kwa muda utakaotumia kwa kumeza kidonge kimoja kila siku. Kuna aina nyingi tofauti ya dawa zilizochangwa na viwango tofauti vya homoni ya estrogen na progestin. Kdonge kilichochanganywa kinachojulikana sana kinaitwa "low-dose" kilicho na mikrogram 20, 30, au 35 ya estrogen. Kidonge cha low-dose na minipills ni tofauti - Vidonge vya lowdose viko na estrogen na progestin ilihali minipills iko na progestin pekee yake. Usitumie kamwe mbinu iliyo na zaidi ya mikrogram 50 ya estrogen.

Mchanganyiko wa vidonge hupatikana katika kliniki za upangaji uzazi, maeneo ya huduma ya afya, duka la dawa na kupitia kwa wahudumu wa afya.

Mara baada ya kuanza kutumia dawa, unapaswa uendelee kutumia aina moja ya bidhaa (na kama unaweza, kununua pakiti kadhaa kwa mara moja). Ikiwa ni lazima ubadilishe aina hiyo ya bidhaa, jaribu kupata nyingine iliyo na jina lile lile la homoni na nguvu. Utakuwa na madhara machache na ulinzi bora.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020422