Nawezaje kuwacha kutumia pombe na mihadarati
1. Kubali kuwa una shida.
2. Amua kufanya jambo LEO.
3. Acha. Ama tumia kidogo kisha uwache. Watu wengi huwacha kutumia mihadarati au pombe mara moja. Inachukua tu mapenzi yao wenyewe na kuamini kuwa wanaweza. Wengine huhitaji usaidizi kutoka kwa kikundi au mipango fulani ya matibabu kama viel Alcoholics Anonymous (AA), ambayo husaidia watu wenye shida za utumizi wa pombe au mihadarati. Kuna mashirika ya AA katika nchi nyingi. Kunaweza pia kuwa na makundi mengine ya matibabu katika maeneo yako. Wanawake wengi huhisi vizuri katika kikundi chenye wanawake pekee. Ikiwa vikundi hivi havipo, jaribu kuanzisha kikundi chako na mtu ambaye ameweza kuwasaidia watu na wakaacha kunywa pombe au kutumia mihadarati.
4. Ukianza kunywa pombe au kutumia mihadarati tena, usijilaumu. Lakini, jaribu kuwacha tena.