Nitavumilia vipi migogoro kuhusu kujamiiana/ngono

From Audiopedia
Revision as of 17:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Hamu ya ngono ni jambo la kawaida, mwanamke anaweza kuhisi hamu ya kujamiiana kama mwanamume. Kimila mwanamke hufunzwa kunyenyekea kwa madai ya kujamiiana na waume wao na kwamba wanawake wazuri hawana hamu yao wenyewe ya kushiriki tendo la ngono. Mafunzo haya ni mabaya na ya kudhuru. Ni vyema na kawaida kwa wanaume na wanawake kushirikiana raha ya tendo la ngono kwa pamoja. Wakati kila mpenzi ataelewa aina ya mazungumzo ya mapenzi na kugusa mahali mwenzako anapenda, wote wanaweza kufurahia kujamiiiana.

Zungumza na mpenzi wako kuhusu ngono. Hii inaweza kuwa ngumu sana ikiwa hujawahi kufanya hivyo hapo awali, lakini ni muhimu sana. Ikiwa hamtazungumza, atajuaje ikiwa unafurahia ngono naye?Mweleze unachokipenda na usichokipenda. Mpenzi wako hawezi kujua vile mwili wako unavyohisi unapoguswa kwani mwili wako na wake ni tofauti na mwili tofauti uhisi hisia tofauti unapoguswa. Mfundishe jinsi ya kukufurahisha.

Tendo la ngono huanza kwa kumbusu, kumshika, kuzungumza au kumwangalia mtu hadi ahisi raha. Huchukua muda kwa mwanamke kufurahishwa hadi kufika kikomo au kuhisi utamu zaidi baada ya kujamiiana ikilinganishwa na mwanamume. Kwa hivyo mweleze mpenzi awe na subira na asiwe na haraka wakati wa kujamiiana.

Inawezekana kwa karibu wanawake wote kuhisi utamu wa kikomo wakati wa kujamiiana, lakini wanawake wengi hukosa kuhisi utamu huo au huhisi utamu huo mara moja moja. Ikiwa anataka, mwanamke anweza kujifunza jinsi ya kupata utamu zaidi, kwa kujigusa au kwa kumruhusu mpenzi wake amguse na kueleza anavyohisi anapoguswa. Kujigusa mwenyewe kunaweza kumfanya mwanamke aelewe mwili wake na miguso ipi humfanya ahisi utamu - kisha atamuonyesha mpenzi wake.

Kiasi cha hamu mwanamke anachohisi hubadilika wakati wa siku za hedhi, au kwa wakati mwingine katika maisha yake. Ikiwa hamtahisi kujamiiana, sameheaneni na mzungumzie suala hilo. Tengeni muda wa kujamiiana wakati mnapotaka, na mfanye mambo ambayo mnafurahia kufanya.

Tendo la ngono halistahili kuwa na uchungu. Uchungu wakati mnajamiiana ni ishara kuwa mambo si sawa. Mwanamke atahisi uchungu wakati wa kujamiiana wakati:-

  • Mpenzi wake ataingiza uume wake kwa uke ikiwa uke haujakuwa na majimaji au kama mwanamke hajatulia
  • Mwanamke atahisi yuko na hatia au kama hataki kujamiiana.
  • Akiwa na maambukizi (Muone mhudumu wa afya kwa usauidiziwa kiafya)
  • Amekatwa sehemu ya siri.

MUHIMU:Ikiwa unashuku au unajua kuwa mumeo si mwaminifu usijamiiane naye hadi akubali kutumia mpira au kondumu. Ikiwa anajamiiana na wengine anaweza kupata maambukizi ya zinaa kama virusi vya ukimwi au ukimwi kisha akuambukize. Wanaumme na wanawake wanaweza kupata magonjwa ya zinaa lakini mwanamke huambukizwa kwa urahisi - kwa hivyo uko kwa hatari kubwa.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw021014