Nawezaje kuzuia magonjwa ya zinaa
Kuzuia magonjwa ya zinaa kunaweza kukulinda wewe na mpenzi wako kutokana na magonjwa hatari na utasa.
Shiriki ngono salama.
Tumia kondomu kila unaposhiriki ngono. Kondomu za kike na za kiume:
Ikiwa mpenzi wako hatatumia kondomu, diaghragm itakulinda kutokana na magonjwa fulani ya zinaa, hasa kisonono na chlamydia.
Osha nje ya uuke wako baada ya kushiriki ngono.
Nenda haja ndogo baada ya kushiriki ngono.
Usitumie miti shamba au poda kukausha uuke wako. Unaotumia maji na sabuni kuosha ndani ya sehemu yako ya uzazi, unaleta hitilafu na namna asilia ya uke wako ambayo huiweka ikiwa na afya. Sehemu yako ya uzazi ikikauka, unaweza kuhisi uchungu wakati wa ngono. Hii hukuweka katika hatar ya kuambukizwa virusi vya HIV na magonjwa mengine ya zinaa.
Wewe na mpenzi wako mnaweza kushiriki aina zingine za kuonyeshana mapenzi badala ya kushiriki ngono.
Msishiriki ngono, ikiwa wewe na mpenzi wako mna ishara za ugonjwa wa zinaa.