Kwa nini nitumie mbinu za upangaji uzazi

From Audiopedia
Revision as of 17:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Mwanamke aliye na umri mdogo anastahili kutumia mbinu za upangaji uzazi kuchelewesha mimba ya kwanza mpaka mwili utakapokomaa kikamilifu. Kisha, baada ya mtoto wa kwanza kuzaliwa, anastahili kusubiri miaka miwili au zaidi kati ya kila mimba. Mbinu hii, inaitwa kupanga watoto vyema, inasababisha mwili wa mama kupata nguvu tena kati ya mimba tofauti na mtoto wake anaweza kumaliza kunyony kwa ukamilifu.

Wakati anapopata idadi ya watoto anaowataka, anaweza kukamilisha uzazi.

Ili kuwa na akina mama na watoto walio na afya, ni vyema kutopata:

  • Watoto mapema sana
  • Watoto kuchelewa sana
  • Watoto wengi
  • Watoto waliofuatana kwa ukaribu sana.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010207