Je nawezaje kuwalinda watoto wangu kutokana na ajali za barabarani

From Audiopedia
Revision as of 17:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Watoto wanaweza kujeruhiwa wakati wanavuka barabara au wakiwa tu wanatembea barabarani au wanapocheza barabarani. Watoto wadogo huwa hawafikirii kabla ya kwenda barabarani.

Ni wajibu wa familia kuhakikisha kuwa:

  • wanawaangalia watoto kwa umakini
  • wanaweka ua kuzunguka nyumba, kufunga lango kuu ili kuzuia watoto wadogo kwenda barabarani
  • wafundishe watoto wadogo kuwa wasivuke barabara, wala kutembea barabarani isipokuwa wakiwa wameambatana na mtu mzima au mtoto aliyewashinda kwa umri
  • watoto hawachezi karibu na barabara
  • wafundishe watoto kuwa wasikimbilie mipira au vifaa vya kuchezea ambavyo huenda karibu na barabara
  • wafundishe watoto kutembea kando kando ya barabara, wakielekea kule ambako magari yanatoka
  • ikiwa kuna njia kando ya barabara, wafundishe watoto kuitumia badala ya kutembea barabarani
Sources