Nitawezaje kuanzisha kikundo changu

From Audiopedia
Revision as of 17:24, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Tafuta wanawake wengine wawili ambao wangependa kuanzisha kikundi.

Panga siku na mahali pa kukutana. Itasaidia sana ikiwa mtapata mahali tulivu kama viel shule, kituo cha afya, au mahali pa sala. Mnaweza kupanga pia kuwa na mkutano wakati wa shughuli za kila siku.

KAtika mkutano wa kwanza, zungumzieni matarajio yenyu. Ikiwa mko katika kikundi, amueni jinsi kikundi kitaongozwa, na ikiwa wanachama wapya wataruhusiwa kujiunga nanyi baadaye. Ingawa aliyeanzisha kikundi atasimamia mikutano ya kwanza, asifanye uamuzi kwa niaba ya kikundi. Jukumu lake ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata nafasi ya kuzungumza na kuhakikisha kuwa mazungumzo hayapotezi mwelekeo. Baada ya mikutano michache ya kwanza, wanachama wanaweza kuchukua zamu kukiongoza kikundi. Kuwa na zaidi ya kiongozi mmoja kutawasaidia akina mama ambao wanaona haya kupata nafasi ya kuongoza.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010310