Nawezaje kuzungumza na mpenzi wangu kuhusu ngono salama
From Audiopedia
Ukiona kuwa mpenzi wako anakuunga mkono katika uamuzi wako wa kushiriki ngono salama, jaribu kuzungumza naye kuhusu madhara ya magonjwa ya zinaa kwa afya. Jambo hili sio rahisi! Wanawake wengi hufundishwa kuwa sio vizuri kuzungumzia mambo ya ngono - hasa na wapenzi wao au wanaume wengine - hivyo basi hawana uzoefu. Mwanaume anaweza kuzungumza na wanaume wengine kuhusu ngono, lakini huona aibu kuzungumza na mpenzi wake. Hapa kuna mapendekezo: