Ninaweza kufanya nini ili kuzuia vurugu isababishwayo na mpenzi wangu

From Audiopedia
Revision as of 17:23, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Mwanamke hana mamlaka kwa vurugu isababishwayo na mpenzi wake, lakini anaweza kuchagua atakavyomjibu. Anaweza pia kujaribu kupanga jinsi atakavyoweza kuwapeleka watoto wake mahali salama hadi pale mwanamume huyo atakapowacha kusababisha vurugu.

Andaa mpango wa usalama, inayojumuisha:

  • Usalama kabla vurugu kutendeka tena.
  • Usalama wakati wa ghasia
  • Usalama wakati utakapo kuwa tayari kuondoka.
Fikiria kuhusu mambo haya hata kama unadhania ya kwamba vurugu haitawahi kutendeka tena. 
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020115