Nawezaje kuimarisha lishe langu

From Audiopedia
Revision as of 17:23, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Hapa kuna mapendekezo machache ya jinsi ya kuimarisha lishe. Mapendekezo haya yatakusaidia kukuza chakula aina tofauti, kukihifadhi vyema ili kisiharibike. Baadhi ya mapendekezo haya huleta suluhisho ya haraka. Mengine huchukua muda mrefu.

Ili kuongeza kiwango cha chakula ambacho shamba lako huzalisha, jaribu kupanda aina tofauti ya vyakula pamoja. Kwa mfano, panda vyakula aina ya vimelea pamoja na vile ambavyo husimama vyenyewe. Miti ya matunda inaweza kupandwa pamoja na vyakula. Au, vyakula vinavyochukua muda mfupi kumea vinaweza kupandwa pamoja na vile ambavyo huchukua muda mrefu kumea.

Chakula cha kwanza kinaweza kuvunwa kabla ya kile cha pili kukomaa.

Ikiwa ni azima upande vyakula vya kuuzwa, jaribu pia upande vyakula visivyo vya kuuzwa. Kwa mfano, panda miti ya matunda ili kuipakahawa kivuli. Au, panda muhogo pamoja na mmea wa pamba.

Jaribu kutafuta mimea ya lishe bora ambayo inapatikana katika eneo lako, ili utumie mbolea na maji kidogo kwa matkeo mazuri.

Kuzungusha mimiea: Kila msimu wa upanzi, panda mimea ambayo inarutubisha udongo - kama vile maharagwe, mbaazi, ndengu, alfalfa, njugu ama aina nyingine ya nafaka. Kwa mfano, mwaka huu panda mahindi, mwaka ujao panda maharagwe.

Jaribu kukuza aina tofaiuti ya vyakula. Hivyo, hata mmea mmoja ukikosa kufanya vyema, utakuwa na chakula.

Mitaro itazuia mmomonyoko wa udongo.

Tumia mbolea asilia. Jitengenezee mbolea hapo shambani, ndio uipate bure.

Ikiwezekana, pamoja na wenzako, anzisheni chama cha wakulima. Jamii inaweza kununua chakula kingi kwa bei nafuu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010423