Vipi kurejelea mizunguko ile ile yaweza kuharibu afya yangu

From Audiopedia
Revision as of 17:23, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Joints ni sehemu katika mwili ambapo mifupa hukutana. Katika eneo hilo ambalo mifupa hukutana, tishu zilizo na nguvu (tendons) huunganisha mifupa kwenda kwa misuli.

Ukirejelea mzunguko uo huo tena na tena ukiwa unafanya kazi, tishu hizo (tendons) zaweza kuharibika. Majeraha ya kigae cha mkono (wrist) na elbows ni ya kawaida kwa wakulima na wafanyikazi wa kiwanda. Majeraha ya magoti hushuhudiwa sana miongoni mwa wafanyikazi wa nyumbani, wachimbaji na wafanyikazi wengine ambao hupiga magoti kwa muda mrefu.

Ishara/Dalili:

  • Maumivu na ganzi katika eneo la mwili wako linalorejelea mzunguko huo.
  • Kwa kigae cha mkono (wrist) utahisi uchungu mkono wako unapoguswa kwa upole
  • Utahisi kama mifupa inakwaruzana ukiweka mkono juu ya joint na kuunzungusha.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030119