Ni vipi ambavyo ninaweza kuhifadhi chakula
Kutumia chungu Hiki ni chungu kidogo ndani ya nyungu kubwa. Nafasi iliyo kati ya vyungu hivi viwili hujazwa maji. Tumia nyungu kubwa na kifuniko chake ambacho hakijapakwa rangi) ili maji yaweze kutoka kwa urahisi. Ni muhimu kuwa chungu kidogokisipakwe rangi kwa ndani ili kukiweka kikiwa safi na kuhakikisha kuwa maji hayaingii kwenye chakula kilichohifadhiwa.
Kutumia kabati
Egesha kreti ya mbao kwa upande, na uiweke juu ya mawe. Weka chombo cha maji juu ya kreti na ufunike kreti hiyo na chombo kile kwa gunia au kitambaa kingine kizito. Funika kreti nzima. Hakikisha kuwa kitambaa kile hakiguzi sakafu. . Tumbukiza kitambaa ndani ya maji, ili unyevunyevu usambae kwenye kitambaa hicho. . Weka chakula ndani ya kreti. Maji yaliyo kwenye kitambaa husaidia kuhifadhi chakula. Mbinu hii huhakikisha kuwa kitambaa kina unyevunyevu.