Nitajuaje ikiwa mtu anaugua kifua kikuu

From Audiopedia
Revision as of 17:23, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Ishara ya kawaida ya kifua kikuu huwa ni kikohozi cha zaidi ya muda wa wiki 3, hasa ikiwa kuna damu kwenye kikohozi chenyewe (kamasi ambayo hutoka kwenye mapafu). Ishara zingine ni kukosa hamu ya kula, kupungua uzani, joto mwilini, uchovu na kutokwa jasho usiku.

Njia pekee ya kujua ikiwa mtu anaugua kifua kikuu ni kufanyia mate yake uchunguzi. Ili kupata sampuli ya kikohozi - na wala sio mate tu - lazima mtu akohoe kutoka ndani ya mapafu. Kikohozi hiki hufanyiwa uchunguzi kwenye maabara, kuona ikiwa kina viini vya kifua kikuu.

MUHIMU: Kwa vile ni jambo la kawaida watu waougua HIV kuambukizwa kifua kikuu, wale wote walioambukizwa virusi vya HIV lazima wafanyiwe uchunguzi wa kifua kikuu. Ikiwa uchunguzi utaonyesha kuwa mtu anaugua kifua kikuu, lazima aanze matibabu mara moja. Katika mataifa ambapo kuna visa vingi vya HIV, watu wte wanaougua kifua kikuu lazima wafanyiwe uchunguzi ikiwa pia wameambukizwa HIV.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011606