Nitalindaje afya yangu ikiwa nimeambukizwa virusi vya ukimwi

From Audiopedia
Revision as of 17:23, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Tafuta mahali ambapo kuna ulinzi na matibabu ya HIV, mara unapogundua kuwa umeambukizwa virusi vya HIV. Bado hakuna tiba ya virusi hivyo, lakini kuna madawa ya kuwasaidia walioambukizwa HIV kuishi maisha marefu na kupata shida kidogo.

Tafuta matibabu mapema. Muone mhudumu wa afya mara kwa mara. Unapougua, hakikisha kuwa unapata matibabu kamili. Ugonjwa wowote ule hupunguza kinga ya mwili.

Kula chakula chenye afya ili mwili wako uwe na nguvu. Vile vyakula ambavyo ni vizuri kuvila wakati uko na afya njema ni vizuri kuvila unapougua. Nunua chakula chenye afya badala ya kutumia pesa kununua dawa za vitamini.

Epuka matumizi ya tumbaku, pombe na mihadarati.

Shiriki ngono kwa njia iliyo salama kwa afya yako na ya mpenzi wako.

Fanya mazoezi na upumzike. Hii itausaidia mwili wako kuweza kupambana na maambikizi na wenye nguvu.

Zuia maambukizi kwa kuoga na kutumia maji safi ya kunywa na kwa kutayarisha chakula.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011011