Nawezaje kuzuia shida za kiafya zinazosababishwa na matumuzi ya maji
From Audiopedia
Maji masafi husaidia watu kuwa na afya bora. Kote ulimwenguni watu wananungana kuboresha afya katika miradi ya maji vijijini mwao. Mara nyingi wanawake hawahusishwi katika mikutano na uamuzi kuhusu miradi hii kama vile pale ambapo mifereji itawekwa, pa kuchimba visima na mfumo utakaotumika.
Ikiwa kijiji chenu hakina maji safi, ungana na wanakijiji wengine katika kupanga mradi wa maji. Ikiwa mnao mradi huo, uliza kwamba wanawake wafunzwe jinsi ya kurekebisha na kutunza mifumo hiyo ya maji.
Kama waishi karibu na mto ambapo kuna kiwanda kinachotupa kemikali majini, jitahidi muungane na wanakijiji wenzako kupata suluhu.