Ni vipi ambavyo tumbaku inaweza kudhuru afya yangu
Watu ambao huvuta sigara huwa waraibu kwa dawa fulani iliyoko kwenye tumbaku iitwayo, nicotine. Wao huhisi wasi wasi au wagonjwa wanapokosa kuvuta sigara. Ni vigumu sana kuwacha kuvuta sigara, kwa sababu nicotine humfanya mtu kuwa na uraibu.
Kwa vile ni wanaume huvuta sigara sana kuliko wanawake, uvutaji sigara umetambuliwa kama shida ya kiafya kwa wanaume pekee. Uvutaji wa sigara umekuwa chanzo cha kuzorota kwa afya ya akina mama. Pia, ni chanzo cha afya mbaya katika mataifa yanayositawi. Mojawapo ya sababu ni kwamba uvutaji sigara husaidia watu kukabiliana na msongo wa mawazo. Sababu nyingine ni kwamba, kampuni zinazotengeneza tumbaku zinajaribu sana kuuza sigara katiak mataifa haya, huku watu katiak mataifa yaliyositawi wakiacha uvutaji wa sigara.
Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha magonjwa kwa wale walio karibu nawe na hawavuti sigara. Watoto wenye wazazi wanaovuta sigara wana maambukizi mengi ya mapafu na hupata shida za pumu wakilinganishwa na watoto ambao wazazi wao hawavuti sigara.
Uvutaji wa sigara unaweza kusababisha:
Baadhi ya shida hizi zinaweza zinaweza kusababisha kifo. Mmoja kati ya watu 4 ambao huvuta sigara watakufa kutokanana na shida inayosababishwa na uvutaji wa sigara.