Ni wakati gani mwafaka wa kuwacha kunyonyesha

From Audiopedia
Revision as of 17:22, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Mtoto yuko tayari kwa lishe nyingine wakati:

  • anapotimiza umri wa miezi 6, au zaidi.
  • anapoweza kujichukulia chakula kutoka kwa meza au akipewa na familia.
  • asiposukuma chakula kwa kutumia ulimi wake

Kati ya miezi 6 na mwaka 1, mnyonyeshe mtoto kila anapohitaji kunyonya. Usimpe vyakula vingine kabla hajafikisha umri wa miezi 4. Hata kama mtoto mwenyewe anakula vyakula vingine, bado anahitaji kunyonyeshwa kama hapo mbeleni. Unavyomnyonyesha, unaweza pia kumpa vyakula vingine, mara 2 au 3 kwa siku. Anza na na chakula chepesi kama vile uji au nafaka. Baadhi ya akina mama huchanganya vyakula hivi kwa kutumia maziwa yao. Hauhitaji nafaka ghali kwa mtoto wako.

Ikiwa mtoto hatatosheka na kunyonyeshwa, na umri wa kati ya miezi 4 hadi 6, labda anahitaji kunyonya zaidi ndivyo matiti ya mama yaweze kutengeneza maziwa zaidi. Lazima mama amnyonyeshe mtoto, akihitaji kwa siku 5 mfululizo. Ikiwa bado mtoto hana raha, basi ajaribu vyakula vingine: pondaponda vyakula vyote hadi vilainike, hadi pale ambapo mwenyewe ataweza kutafuna. Tumia kikombe au bakuli na kijiko kumlisha mtoto wako.

Watoto wanahitaji kula kila mara - angalau mara 5 kwa siku. Kila siku, ni lazima wapate chakula kama vile uji, mahindi, ngano, mtama, viazi na mhogo, ukiwa umechanganywa na vyakula vya kujenga mwili kama vile maharagwe, njugu, mayai, jibini, nyama au samaki, matunda na maboga, na vyakula vya kuupatia mwili nguvu kama vile njugu, kijiko cha mafuta ya kupika na majarini. Hauhitaji kupika mara 5 kwa siku. Vyakula vingine vinaweza kulika vikiwa baridi.

Ongeza vyakula vipya, moja baada ya kingine. Mtoto atakapofikisha miezi 9 au mwaka 1, mtoto ataweza kula vyakula vikiwa vimekatwa kwa vipande vidogo vilivyo rahisi kula.

Katika mwaka wa pili, maziwa ya mama yanaendelea kumpa mtoto kinga kutokana na maambukizi na shida zingine za kiafya. . Ikiwezekana, endelea kumnyonyesha mtoto hadi atakapofikisha angalau miaka 2, hata kama una mtoto mwingine. Mara nyingi watoto wenyewe huwacha kunyonya.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010807