Ninawezaje kupata maji safi ya kunywa
From Audiopedia
Hakikisha kuwa nyumba ni safi na umeweka maji ya kunywa kwenye vyombo safi na uvifunike.
Hakikisha kuwa umeteka maji ya kunywa kutoka kwenye chanzo kilicho safi. Ikiwa maji ni machafu, yaache yatulie, kisha mwaga yale masafi kwenye chombo tofauti. Kabla ya kunywa, ua viini hatari kwa kuyasafisha kama ilivyoelezwa hapo chini.
Weka maji yaliyosafishwa kwenye vyombo safi na uvifunike. Ikiwa chombo kilitumika kuweka mafuta ya kupikia, hakikisha kuwa umekiosha vyema kwa kutumia sabuni na maji moto kabla ya kuweka maji safi. Usiweke maji ndani ya vyombo ambavyo vimetumika kwa kuweka kemikali au dawa za kuua wadudu au petroli. Osha vyombo vya kuhifadhi maji kwa kutumia sabuni na maji safi angalau mara moja kwa wiki.