Nawezaje kudhibiti ugonjwa wa kisukari
Ikiwa unaugua Aina 2 ya ugonjwa wa kisukari, muone mhudumu wa afya ili aweze kuchunguza viwango vya sukari kwenye damu yako, kuona ikiwa unahitaji dawa. Unaweza kudhibiti ugonjwa wa kisukari kwa kula vyema.
Ikiwezekana, hakikisha kuwa unamuona mhudumu wako wa afya kila mara kuhakikisha kuwa ugonjwa haujafika kiwango kibaya.
Ili kuzuia maambukizi na majeraha kwenye ngozi, sugua meno baada ya kula, oga na uvae viatu kuepuka majeraha miguuni. Kagua mikono na miguu yako mara moja kwa siku kuona ikiwa una vidonda. Ikiwa una kidonda na kuna ishara ya maambukizi (ni nyekundu, kimefura au kina joto) muone mhudumu wa afya.
Ikiwezekana, weka miguu juu unapopumzika. Hii inasaidia sana hasa ikiwa miguu yako inapoteza rangi na kuwa nyeusi au kufa ganzi. Hii ni ishara kuwa damu haitembei sawa sawa kwenye miguu miguu yako.