Nini husababisha maambukizi ya figo na ya kibofu cha mkojo
From Audiopedia
Maambukizi ya njia ya mkojo husababishwa na viini. Viini hivi huingia mwilini kupitia sehemu ndogo iliyo chini ya sehemu ya uzazi ya mwanamke. Maambukizi haya kwa kawaida huwashika sana wanawake kuliko wanaume kwa sababu mshipa wa kupitisha mkojo katika maumbile ya wanawake, ni mfupi. Viini hupanda kwa urahisi kupitia kwenye mshipa huu na kuingia kwenye kibofu cha mkojo.