Nini ishara za utumizi mbaya wa pombe na mihadarati

From Audiopedia
Revision as of 17:21, 18 July 2023 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Ni rahisi sana kwa pombe na mihadarati kutumiwa vibaya, haijalishi ni kwa sababu gani. Mtu husemekana kutumia pombe au mihadarati vibaya ikiwa atashindwa kujidhibiti, kiwango anachotumia au tabia yake anapotumia pombe na mihadarati.

Hapa kuna ishara kuwa mtu anatumia pombe na mihadarati vibaya. Yeye:

  • anahisi anahitaji kinywaji au mihadarati mchana au usiku. Ataitumia kwa wakati na mahali pasipofaa, kama vile asubuhi, au akiwa peke yake.
  • atadanganya au kuficha habari kuhusu kiwango yeye na wenzake hutumia.
  • atakuwa na shida za pesa kwa sababu ya kiwango cha pesa yeye hutumia kwa kununua pombe au mihadarati.
  • ataharibu sherehe kwa sababu ya kiwango cha pombe anachokunywa au mihadarati anayotumia.
  • anaona haya kwa sababu ya utumizi wake wa pombe na mihadarati.
  • ana shida na tabia ya kuleta vurugu. Huenda Mwanaume aanze vurugu dhidi ya mkewe, watoto na marafiki.

Ikiwa utumizi wa mihadarati unabadilisha maisha yako, itabidi upunguze au uwache kabisa. Afadhali kuwacha kabla mihadarati hiyo haijakudhuru wewe, familia au marafiki zako.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010304