Utakusanya aje maji ya mvua katika vyanzo vya ardhi

From Audiopedia
Revision as of 18:26, 14 March 2025 by Marcelheyne (talk | contribs) (XML import)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)
Jump to: navigation, search

Mashimo ya ardhini ni njia mojawapo ya kukusanya maji ya mvua. Kwani, hufanya kazi kwa kukamata maji kutoka kwa mvua (kwa mfano kutoka barabarani) katika eneo la kina kifupi au bonde. Ili kutengeneza kisima cha maji, chimba shimo la kina kirefu ardhini na ugonge chini ardhini au lainisha kwa udongo, vigae, zege au karatasi ya plastiki. Hifadhi hii inaweza kutoa maji kutumika na wanyama, kwa umwagiliaji au kwa shughuli kama kuoga. Ikiwa utataka kutumia maji haya kwa ajili ya kunywa, ni bora kuzingira eneo hilo ili kuwazuia wanyama, kwani wanaweza kuchafua maji. Barabara za lami huzalisha maji mengi zaidi kuliko barabara za udongo lakini maji hayo yanaweza kuwa na viambata vya lami hatari kwa watu na mifugo na kwa hiyo yanapaswa kutumika kwa umwagiliaji pekee.

Maji yanayokusanywa kutoka kwenye paa au vyanzo vya maji yanaweza pia kuelekezwa kwenye matangi ya chini ya ardhi. Kuhifadhi maji chini ya ardhi ni njia nzuri ya kuweka maji baridi na kufunikwa. Inaweza kuwa na gharama ya chini kuliko kujenga au kununua matangi ya kuwekwa juu ardhini. Hifadhi ya chini ya ardhi inaweza kuwa suluhisho la bei nafuu kwa kuweka usambazaji wa maji salama na thabiti.


Sources
  • Audiopedia ID: Sw3121