Virusi vya ukimwi ni nini

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Hivi ni vidudu vidogo, vinavyoitwa virusi ambavyo huwezi kuviona. Ukimwi ni ugonjwa ambao hukua baadaye, baada ya mtu kuambukizwa na virusi vya ukimwi.

Wakati mtu anapoambukizwa na VVU, hushambulia mfumo wa kinga, sehemu ya mwili ambayo hupigana na maambukizo. Virusi hivi kwa utaratibu huuwa seli za mfumo wa kinga mpaka mwili unashindwa kujikinga kutokana na maambukizo mengine.

Watu wengi wanaoambukizwa huwa si wagonjwa kwa muda wa miaka 5 kueleka 10. Lakini mfumo wa kinga hauwezi kupigana na maambukizi ya kawaida. Kwa sababu virusi vya ukimwi huchukua miaka kufanya mtu kuwa mgonjwa, watu wengi walio na virusi hivyo hujihisi wa afya na hawana habari kwamba wana virusi hivyo.

MUHIMU: Virusi vya Ukimwi vinaweza kuenezwa kwa wengine pindi tu mtu anaambukizwa, hata kama unamtazamo na hisia za afya njema. Hauwezi kujua ikiwa mtu aanavyo virusi hivi unapomwangalia. Ile njia pekee ya kujua kama ameambukizwa ni kwa kupimwa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011002