Vipi ambavyo nitapika chakula vizuri

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

  • Kupika chakula huua viini. Ni muhimu kupika nyama zote, samaki na kuku vizuri. Chakula kisiwe kibichi wala kuwa na rangi ya kuonyesha kuwa ni kibichi.
  • Chakula kinapoanza kupoa, vile viini huanza kumea tena. Ikiwa chakula hakitaliwa katika mda wa masaa 2, kipashe moto hadi kiwe moto kabisa. Vyakula maji maji lazima vichemke, na vyakula vigumu kama mchele lazima vitoe mvuke.
  • Kuna jamii fulani ambazo hutayarisha nyama na samaki kwa kutumia mbinu za kitamaduni ili iwe salama kwa kula.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010122