Utajuaje iwapo maji ni masafi

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Maji ni muhimu katika jamii. Upatikanaji wa maji safi ya kutosha ni jambo muhimu kwa afya ya jamii. Watu wanapofanya maamuzi kwa pamoja jinsi ya kukusanya, kuhifadhi, na kutumia hifadhi zao za maji vyema watahakikisha kwamba kuna hifadhi ya kutosha ya maji katika jamii.

Watu wengi wako tayari kufanya linalohitajika ili mradi wapate maji safi ya kutosha. Katika sehemu nyingi ambazo watu wanahitaji maji ya kunywa, huenda maji hayo yakawa machafu au yaliyo na vijidudu, minyoo, au kemikali zilizo na sumu, au yanachukuliwa na viwanda au kuuzwa kwa bei ambayo watu hawawezi kumudu.

Ni vigumu kujua iwapo maji ni salama kwa matumizi au la. Baadhi ya mambo ambayo husababisha matatizo ya afya huonekana kwa urahisi kwa kuangalia, kunusa, au kuonja, Lakini maji yanaweza kuwa na viini hatari vinavyoleta madhara bila kuonekana ,kunusa au kuonja. Haya yanaweza kugunduliwa tu iwapo maji yatapimwa. Upimaji wa maji kwa mara nyingi hufanywa kwa kuchunguza sampuli za maji katika maabara. Vipimo hivyo huonyesha aina na kiasi cha uchafuzi kwa kupata chembechembe za kemikali. Upimaji huo ni wa gharama, kheri kufunza jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa maji na mazingira yake.

Ili kuzuia matatizo ya kiafya, ni vyema kuelewa chanzo cha maji machafu na kuchukua hatua mwafaka za kuzuia uchafuzi wa maji.

Sources
  • Audiopedia ID: Sw3102