Unyunyizaji maji shambani ni nini

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Njia ya kunyunyiza maji shambani ni mfumo mzuri wa umwagiliaji maji ambao hupeleka maji moja kwa moja kwenye mizizi ya mmea.

Katika sehemu nyingi duniani, umwagiliaji maji shambani ni mojawapo ya jambo la lazima katika uzalishaji wa mazao. Pamoja na mvua kunyesha, baadhi ya mazao bado huhitaji umwagiliaji maji haswa katika maeneo kame na maeneo makavu. Maeneo yanayo shuhudia joto kali na hali ya hewa kavu yanaweza kuwa changamoto kubwa kwa maendeleo na ukuzaji wa mimea. Japo Unyunyizaji maji shambani ni muhimu, utumizi wa maji mengi unaweza kuleta matatizo kama vile kuharibu mchanga, mizizi, maji kujaa kupita kiasi, chumvi nyingi kwenye eneo la mizizi na pia kupunguza ubora wa mimea na mavuno.

Unyunyizaji maji shambani ni mojawapo ya njia za umwagiliaji maji ambao unaweza kuokoa pesa za wakulima na kuongeza mavuno yao. Unyunyizaji maji shambani ni aina ya umwagiliaji maji ambao huokoa maji kwa kupeleka maji polepole kwenye ukanda wa mizizi ya mimea. Kwa hivyo ili kuhakikisha kuwa kuna ukuzaji sahihi wa mimea na mavuno mengi, mtu anaweza kutumia njia hiyo shambani.


Sources
  • Audiopedia ID: Sw3110