Unawezamkuzuia kusambaa kwa virusi vya ukimwi kwa njia zifuatazo
From Audiopedia
Ikiwezekana, shiriki ngono na mtu mmoja pekee, ambaye pia anashiriki ngono wa wewe pekee.
Shiriki ngono salama - ngono ambayo huzuia shahawa, damu na umajimaji wa sehemu za uzazi za mwanamke kuingia kwenye njia ya haja kubwa, au mdomo. Tumia mipira kwa njia inayostahili kila unaposhiriki ngono.
Hakikisha kuwa unapimwa virusi vya HIV na kupata matibabu ya magonjwa ya zinaa, na hakikisha kuwa wapenzi wako pia wanatibiwa.
Usijidunge sindano wala kujikata ngozi na vifaa ambavyo havijasafishwa baada ya kutumiwa.
Epuka kuongezewa damu isipokuwa wakati wa dharura.
Usishirikiane nyembe.
Usishike damu ya mtu mwingine, wala kidonda chake bila kinga.