Ugonjwa wa TB huenea aje
From Audiopedia
TB huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine wakati ambapo mtu aliyeambukizwa anakohoa vidudu hewani. Wadudu wanaezaishi hewani kwa muda wa masaa kadhaa.
Watu walioambukizwa TB mapafuni wanaeza eneza wadudu kwa wengine. Wamama wakiambukizwa TB, kuna uwezekano wa kuambukiza watoto wao na wale wengineo walio chini ya huduma yao kila siku. watu walio na ugonjwa wa TB lakini hawana ishara yake na wale waliowagonjwa kwa sehemu zingine za mwili hawana uwezo wa kuambukiza.
Mtu asipotibiwa vilivyo, anaweza kuambukiza watu zaidi ya kumi kila mwaka lakini wakati mtu anapotibiwa na amekuwa akikunywa dawa kwa muda wa mwezi mmoja, pengine hana uwezo wa kuambukiza wengine.