Ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia ni nini
Ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia yamaanisha kitendo cha ngono ambacho mwanamke hataki. Ubakaji ni pale mwanamume anapoweka uume wake, kidole, au kitu chochote ndani ya uke wa mwanamke, shimo la haja kubwa, au mdomo bila ridhaa ya mwanamke.
Ubakaji wakati mwingine unajulikana kama unyanyasaji wa kinjinsia kwa sababu ni tendo la mabavu (nguvu), kutumia jinsia kama kinga. Unyanyasaji wa kijinsia unahusisha ubakaji pamoja na aina zote za ngono zisizotarajiwa.
Baadhi ya watu hufikiria kwamba kulazimisha kitendo cha ngono ndio kubakwa tu. Ikiwa mwanamume amempiga mwanamke na kumwacha hajitambui, hufikiria mwanamke angejaribu kujiokoa na hatari ya kuuliwa kuliko kubakwa.
Lakini hata kama mwanamke hatopambana bado ni ubakaji. Haijalishi nini ataamuwa kufanya, kama haikuwa chaguo lake, ni ubakaji na sio makosa yake. Ubakaji ni ukatili wa kijinsia. Wanawake hawapaswi kulaumiwa kwa hili.