Nitazuiaje shida za kiafya zinazoambatana na kemikali

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ili kuzuia hatari za kiafya kutokana na kufanya kazi ukitumia kemikali jaribu kufanya yafuatayo:-

  • Epuka kutumia kemikali kwa ngozi yako. Ukitumia kemikali nyumbani kwako, tumia glavu za jikoni (au mifuko ya plastiki). Ukitumia kemikali kazini, ikiwemo shambani, tumia glavu nzito nauvae viatu. La sivyo, kemikali zitaingia ndani ya mwili wako.
  • Nawa mikono baada ya kutumia kemikali. Ikiwa umekuwa ukitumia kemikali kali, kama dawa ya wadudu, badilisha nguo zako kisha oga kabla ya kula au kuingia ndani ya nyumba. Tumia glavu unapoosha nguo hizo.
  • Usipumue hewa ya mafusho ya kemikali. Fanya kazi mahali kuna hewa safi. Nguo au karatasi ya kujizuia hazitakusaidia kutopumua hewa ya mafusho ya kemikali.
  • Weka kemikali mbali na chakula. Usitumie makopo ya kemikali kuweka chakula au maji hata baada ya kuosha. Kopo linaloonekana safi laweza kuwa na kemikali ya kutosha kufanya chakula au maji kuwa na sumu. Usitumie kemikali karibu na chakula wakati kuna upepo mwingi.

Ikiwa utaingiliwa na kemikali kwa macho, osha haraka iwezenavyo ukitumia maji. Osha kwa dakika kumi na tano. Hakikisha hayo maji yasiingie kwa jicho lako lingine. Ikiwa jicho limeunguzwa na kemikali, muone mhudumu wa afya. Weka kemikali mbali na watoto.

Angalia tahadhari za sumu kwa karatasi iliyobandikwa kwa chupa ya kemikali.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030114