Nitazuiaje shida ya kukosa kwenda haja kubwa

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Uja uzito huufanya mwili kufanya kazi pole pole. Hii husababisha haja kubwa kuwa ngumu, hivyo basi inakjwa vigumu kwenda haja kubwa kwa urahisi.

Ili kuzuia hayo, unahitaji:

  • Kunywa angalau glasi 8 za maji kila siku.
  • Fanya mazoezi kila mara.
  • Ikiwa unatumia tembe za kuongeza damu mwilini, jaribu kumeza tembe moja tu pamoja na tunda au maji ya mchungwa. Au usimeze kwa siku kadhaa.
  • Kula matunda na mboga kwa wingi, ikiwemo chakula kilicho na 'fibre' - kama vile nafaka na muhogo.
  • Usimeze dawa za kurahisisha choo chako. Dawa hizi hufanya kazi kwa muda tu na wala hazimalizi shida hiyo.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010711