Nitazuiaje kufura kwa miguu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ni jambo la kawaida kufura miguu wakati wa uja uzito - haswa kwa wanawake ambao lazima wasimame mchana kutwa.

Namna ya kuzuia:

  • Weka miguu yako juu mara kadhaa ikiwezekana kwa siku.
  • Wakati unapopumzika, lala kwa upande wa kushoto.
  • Ikiwa miguu yako imefura sana, au imefura wakati unapoamka asubuhi, au mikono na uso wako umefura, hizi ni ishara za hali ya hatari hasa ukiwa mja mzito. Muone mhudumu wa afya au nenda hospitalini.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010715