Nitawezaje kuvumilia shida za kuwacha utumizi wa pombe na mihadarati
From Audiopedia
Mtu anapokuwa na uzoefu wa kunywa pombe au kutumia mihadarati kisha awache, atapitia vipindi vingi vya shida zinazotokana na kuwacha. Wakati huo wote, lazima mwili wake uzoee kutotumia mihadarati.
Inaweza kuchukua hadi siku 3 kwa ishara nyingi za kuwacha kunywa pombe kuisha. Watu wengi hawapati shida zozote katika siku hizi tatu, lakini kuna wengine ambao hupata ishara hatari sana. Ni jambo la muhimu mtu kama huyu kupata usaidizi.