Nitawezaje kuimarisha maisha yangu ikiwa nimeambukizwa HIV

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Hakuna yeyote - ikiwe ni wanasayansi au madaktari wa kienyeji - walio na tiba ya HIV. Lakini, wale walioambukizwa HIV wanaweza kuwa na afya njema kwa miaka mingi, hasa watunzwa vyema na kupata matibabu. Wakati huu, itakuwa vyema ikiwa:


Utaishi maisha kikamilifu.

Utakaa na familia na marafiki.

Fanya kazi kama kawadia.

Unaweza kushiriki ngono.

Tumia kinga unaposhiriki ngono. Hii itakulinda wewe na mpenzi wako.

Jiunge, au unda kikundi cha watu wanaougua kutokana na HIV na UKIMWI. Baadhi ya watu walio na HIV na UKIMWI hufanya kazi kwa pamoja ili kuelimisha jamii, kutoa huduma za ulinzi kwa wale ambao wanaugua UKIMWi, na kupigania haki za watu walio na HIV na UKIMWI.

Chunga afya yako ya kiroho na ya kiakili. Imani yako na itikadi zinaweza zikakupatia nguvu na matumaini.

Fikiria kuhusu siku za usoni. Ikiwa una watoto:

  • kaa nao ukiwalinda na kuwapa mawaidha.
  • fanya miapango na familia yako ili wawalinde wakati hautaweza kuwalinda.
  • Ikiwa una pesa umewekeza, nyumba au mali, jaribu kuhakikisha kuwa umeandika kuwa ungependa iwaendee. Wakati mwingine wanawake ambao hawajaolewa kisheria hawawezi kuwaachia watoto au jamaa wao mali. Ni vyema ikiwa utaolewa kisheria ili uweze kuwaachia mali wale ambao utawachagua.

Ikiwa mpenzi wako ana virusi vya HIV: Ikiwa mtashiriki ngono kwa njia salama, mtu aliyeambukizwa anaweza kuepuka kumuambukiza mpenzi wake. Mipira ni njia nzuri ya kuzuia HIV. Funika vidonda na upate matibabu kwa magonjwa ya zinaa. Kumbuka kuwa, kuna njia nyingi za kuhisi tendo la ngono isipokuwa kushiriki ngono.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011010