Nitajikinga vipi na shida za kiafya za kuketi au kusimama kwa muda mrefu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Tembea kiasi kwa haraka wakati wa mapumziko yako. Pia, jaribu kutembea chumbani au angalau jinyooshe kila baada ya saa moja.

Ikiwa itawezekana vaa soksi au soksi zilizo na mkanda. Soksi zifike magotini.

Fanya mazoezi yaliyoko hapa wakati wowote utakapohisi ugumu au uchungu, au kushuka mbele. Rudia mazoezi haya mara mbili au tatu, polepole huku ukipumua ndani na nje kwa muda mrefu:

  • Zungusha kichwa chako polepole kwa mviringo.
  • Zungusha mabega yako juu chini, mbele nyuma, unganisha upande wa nyuma wa mabega yako kwa pamoja.
  • Mgongo wako ukiwa wima, geuka kutoka kwa hip kuaangalia upande. Unapaswa usaidike kutoka sehemu ya juu ya mgongo na ya chini.

Ikiwa unakaa kazini:

  • Kaa kwa kiti kilichonyooka, kilichowima--na kichwa, shingo na mabega viwe wima. Ikiwa utahisi vizuri, weka kitambaa kilichokunjwa au pillow nyuma yako kusaidia sehemu ya chini ya mgongo.
  • Ikiwa itawezekana sawazisha urefu wa kiti au meza kukusaidia ufanye kazi katika hali nzuri. Unaweza kujaribu kukaa juu ya pillow, au kuweka dawati au meza juu ya vitalu.
  • Usiweke mguu wako juu ya mguu mwingine.
  • Epuka kuvaa nguo zinazokubana sana.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030118