Nini umuhimu wa madini aina iron kwa mtoto wangu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Ukosefu wa madini aina iron ndio chanzo cha ukosefu wa damu mwilini. Watoto pia wanaweza kuugua kutokana na ukosefu wa damu mwilini kutokana na malaria au minyoo. Ukosefu wa madini aina iron unaweza kusababisha ulemavu na shida za kiakili katika watoto wachanga na watoto wadogo. Ukosefu wa damu mwilini ndio ugonjwa kawaida sana ulimwenguni.

Watoto wanahitaji chakula chenye madini aina iron ili kuikinga miili na akili zao na kuzuia ukosefu wa damu mwilini. Chanzo kizuri cha madini aina iron ni maini, nyama na samaki. Pia hupatikana kwenye vyakula kama kunde. Vyakula kama vile ngano na unga wa mahindi, chumvi, supu ya samaki au soya huwa zimetiwa madini aina iron. Vyakula na tembe zenye madini aina iron husaidia kuzuia ukoefu wa damu mwilini. Ni muhimu kuvila vyakula hivi pamoja na matunda yenye vitamini C ili mwili uweze kufyonza madini aina iron vyema.

Sources