Wakati wa huduma ya kabla ya kujifungua, mkunga au mhudumu wa afya atakuuliza kuhusu mimba ambazo umekuwa nazo hapo mbeleni, watoto uliowazaa, na kama ulikuwa na shida zozote kama vile kuvuja damu, au watoto waliokufa. Habari hii huwasaidia kujitayarisha kwa lolote lile:
Mkunga anaweza:
Kuhakikisha kuwa mwanamke anakula vyema na pia kumpa mawaidha jinsi ya kula vyema.
Kukupatia tembe za kuongeza damu na zile za folic, ambazo zitazuia upungufu wa damu mwilini na ulemavu wa mtoto
Kumkagua mama mjamzito, ili kuhakikisha kuwa ana afya njema na kwamba mtoto anakua vyema.
Kumpatia mama chanjo ya kuzuia peopunda, ugonjwa ambao unaweza kuwaua akina mama na watoto.
Kukupatia dawa za kuzuia malaria, ikiwa ugonjwa huu ni huathiri eneo hilo.
Kufanya uchunguzi wa virusi vya ukimwi, kaswende na magonjwa mengine ya zinaa.
Kukumpatia mama madawa ya kuzuia mtoto kuambukizwa virusi vya ukimwi na mamake.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.