Ninawezaje kuzuia kichefuchefu
From Audiopedia
Ingawaje huitwa 'ugonjwa wa asubuhi', unaweza kuhisi kutapika wakati wa uja uzito wakati fulani wa siku au hata siku nzima. Hisia hii hupotea mwisho wa mwezi wa 3 au wa 4.
Namna ya kuzuia kichefuchefu:
TAHADHARI: Muone mhudumu wa afya ikiwa unatapika kila unapokula, au kama unapoteza uzani. Angalia ishara za upungufu wa maji mwilini kama vile: kiu, kukosa haja ndogo, mdomo uliokauka, kuhisi kizunguzungu unaposimama, ngozi kukauka. Ikiwa una ishara hizi, na pia unatapika, unahitaji kupewa maji kwa sindano yaani IV. Tafuta huduma ya kimatibabu haraka iwezekanavyo. Kupungua kwa maji mwilini ni hali ya dharura.