Ninawezaje kujitetea mwenyewe - Audiopedia
Fanya mazoezi haya ya ulinzi ya kujitetea ukiwa na rafiki yako, ndiposa uwe tayari kupigana na mshambulizi.
Mpige kwa nguvu unavyoweza. Usioogope kumuumiza- kwani yeye haogopi kukuumiza.
Ikiwa utashambuliwa kutoka nyuma.
- Mgonge ukitumia nguvu kwa tumbo lake ukitumia elbow yako.
- Mkanyage mguu wake ukitumia kisigino chako cha mguu.
- Tumia mkono wako, kushika korodani zake (mipira), kisha zifinye kwa nguvu.
- Ukitumia kisigino chako, mpige teke kwa nguvu chini ya mguu wake au goti.
Ikiwa utashambuliwa kutoka mbele
- Ukitumia vidole vyako mdunge macho yake.
- Tengeneza ngumi kwa mikono yako miwili na umgonge sehemu zote mbili za upande wa kichwa chake, au juu ya masikio yake.
- Tengeneza ngumi kisha umgonge ukitumia nguvu juu ya pua lake.
- Inua magoti, na usukume kwa haraka kama unaweza katika korodani zake (mipira).
Njia zingine za kujitetea ni:
- Ikiwa uko katika eneo la umma kisha mtu ajaribu kukuumiza au kukunyanyasa, piga kelele kwa sauti kubwa uwezavyo.
- Fanya jambo litakalomkera kama vile kutema tema mate, au jifanye unatapika, au fanya jambo la kiuwendawazimu.
- Ikiwa anayekunyanyasa ni jamaa wa famili yako, jaribu kuzungumza kuhusu suala hilo na jamaa mwingine wa familia unayemwamini.
Sources
- Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
- Audiopedia ID: sw020311