Ninapaswa kujua nini kuhusiana na uhusiano wangu wa kimapenzi baada ya kubakwa

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Unaweza kuendelea na uhusiano wako wa kimapenzi wa kawaida baada ya kubakwa. Unahitaji kusubiri hadi sehemu yako ya siri ipone Kwa wanawake wengi, kitendo cha ngono huwafanya wakumbuke walivyobakwa. Kama hili litatendeka kwako, zungumza na mpenzi wako kwanini mnastahili kusubiri.

Wakati mwingine, mpenzi wa mwanamke aliyebakwa anaweza kumkataa. Anaweza kuhisi aibu au afanye kitendo kinachoonyesha kuwa amekasirishwa na mwanamke wake. Jambo hili laweza kuwa gumu kwa mwanamke anayepitia hisia kadhaa ngumu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020320