Nifanyeje kuhakikisha ninapata madini ya calcium ya kutosha

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

kila mtu anahitaji madini ya calcium kufanya mifupa na meno yake yawe na nguvu. Haswa, wanawake na wasichana wanahitaji madini ya calcium zaidi.

Wakiwa watoto. Wasichana wanahitaji madini ya calcium kusaidia mwili kuwa vyema ili wakati wa kujifungua wajifungue kwa urahisi.

Wakati wa Uja uzito. Mwanamke mja mzito anahitaji madini ya calcium kuwezesha mtoto wake aliye tumboni awe na mifupa iliyo na nguvu, vile vile mifupa yake na meno yake yatakuwa na nguvu.

Wakati wa kunyonyesha. Madini ya caldium husaidia kutengeneza maziwa ya mama.

Unapokuwa endele kuzeeka. Madini ya calcium huzuia mifupa kuwa hafifu.

Hizi hapa ni baadhi ya chakula zilizo na madini ya calcium:

  • Maziwa
  • Mifupa
  • Mboga
  • Jibini
  • Simsim
  • Lozi
  • Maharagwe
  • Ndimu/ Chokaa
  • Aina ya samaki ya 'shellfish'

Unapotaka kuongeza madini ya calcium kwa chakula:

Lowesha mifupa au kombora ya mayai ndani ya maji ya siki ama limau kisha utumie maji hayo kupikia.

Nyunyuzia maji ya limau, siki ama tomato wakati wa kupika supu ya mifupa. Unaweza saga makombora ya mayai kisha changanya na chakula.

Lowesha mahindi ndani ya chokaa.

Miale ya jua hukusaidia kutumia madini ya calcium vyema. Kaa angalau dakika kumi na tano kila siku kwa jua. Kumbuka kwamba haitoshi tu kukaa nje. Sharti ngozi yako ipate miale ya jua.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010408