Ni vipi nitawezakuviosha vifaa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya HIV

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Hatua ya 1 na ya 2 lazima zifanywe baada ya kutumia vifaa. Jaribu sana damu na kamasi zisikaukie kwenye vifaa hivi. Hatua ya 3 lazima ifanywe kabla ya kutumia vifaa. HAtua zote zinaweza kufanywa kwa pamoja ikiwa unaweza kuviweka vifaa kama vimeoshwa.

1. Kuweka kwenye beseni la maji Weka vifaa vyako kwenye beseni la maji kwa dakika 10. Ikiwezekana, tumia asilimia 0. 5 ya 'chlorine'. Unapoviweka vifaa vyako ndani ya maji yenye 'chlorine' inasaidia kukukinga kutokana na maambukizi unapoviosha vifaa vyenyewe. Ikiwa hauna 'chlorine', viweke vifaa vyako kwenye maji tu.

2. Kuosha Osha vifaa vyote kwa maji ya sabuni na brashi hadi kila kifaa kionekane safi, kisha usuze vifaa hivyo kwa maji safi. Tahadhari sana usije ukajikata kwa makali ya vifaa hivi unapoviosha. Ikiwezekana, tumia glavu nzito, ama zozote ambazo unazo.

3. Kuosha zaidi Tumia mvuke au chemsha vifaa kwa dakika 20 (sawa na muda unaotumia kupika mchele).

  • Unahitaji sufuria na kifuniko. Sio lazima maji yafunike hivyo vifaa, lakini tumia kiasi cha maji ambayo yataendelea kutoa mvuke kwa dakika 20.
  • Ili kuchemsha vifaa, sio lazima ujaze sufuria na maji. Hakikisha kuwa maji yanafunika kila kitu wakati wote. Ikiwezekana, funika sufuria.

Kwa kuchemsha na kwa kutumia mvuke, anza kuhesabu dakika 20 baada ya maji kuanza kuchemka. Usiongeze chochote kwenye sufuria ukishaanza kuhesabu.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011008