Ni vipi kufanya kazi mbali na nyumbani kunaweza kuharibu afya yangu

From Audiopedia
Jump to: navigation, search

Wanawake wengi hufanya kazi mbali na manyumbani mwao. Wanawake wengine husafiri kila siku kutoka nyumbani hadi kazini, huku wengine wakisafiri maili/masafa marefu ili kuishi karibu na mahali wanapofanyia kazi. Hii yaitwa 'uhamiaji'.

Wakati mwingi wanawake huhama kutoka vijijini kuelekea Jijini ambako viwanda vikubwa vinaweza kuwapa kazi/ajira, au wanapoweza kupata kazi kama wafanyikazi wa nyumbani. Wanawake wengine huamuwa kuhama, lakini wengine hulazimika kuhama kwa sababu ya kukosa chakula au kazi nyumbani, au kwa sababu viwanda hupeana pesa zaidi. Pesa hizo ambazo wanawake hupata ni muhimu sana kusaidia mahitaji ya familia zao manyumbani mwao.

Wanawake wanapohama, huhisi upweke mwanzoni. Hii yaweza kuwatisha, kwa sababu wako mbali na familia na marafiki waliowasaidia.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw030128