Ni vipi futari ya sumu lead poisoning yaweza kuharibu afya yangu
From Audiopedia
Futari au lead ni chembechembe za sumu zipatikanazo katika bidhaa za kawaida - kama udongo wa nyungu, rangi, mafuta ya taa na Batteries. Futari ya sumu hutokea wakati watu wanapokula kutoka kwa nyungu ambazo ziko na vipande vidogo vidogo vya futari au wanapokula kiasi kidogo cha vumbi iliyochanganyikana na futari. Inaweza kutokea kwa kupumua vumbi iliyo na futari au kupumua hewa ya mafusho iliyo na futari.
Futari au (Lead) hudhuru afya ya watoto. Inaweza kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na uzito wa chini, ukuuaji usio bora, kuharibika kwa ubongo( ambayo yaweza kuwa ya kudumu) na kifo. Kwa hivyo ni muhimu kuepuka kufanya kazi palipo na futari wakati wa ujauzito.