Ni vipi ambavyo naweza kuyalinda meno yangu
From Audiopedia
Ni jambo muhimu kuyalinda meno yako kwa sababu:
Ni muhimu kusafisha meno vizuri mara mbili kwa siku. Hii huondoa viini ambavyo husababisha kuoza na kupotea kwa meno. Safisha meno ya mbele na yale ya nyuma, na pia katikati ya meno na kwenye ufizi. Tumia mswaki ulio mwororo, kijiti chembamba au kitambaa. Dawa ya meno ni nzuri lakini sio lazima. Unaweza pia kutumia chumvi, magadi au maji.