Ni vipi ambavyo Virusi vya ukimwi havisambazwi - Audiopedia
Virusi vya ukimwi haviwezi kuishi nje ya mwili wa binadamu kwa muda mrefu. Haviwezi kuishi hewani au kwenye maji.
Hii inamaanisha huwezi kupata virusi vya ukimwi kwa njia zifuatazo:
- kwa kumshika mtu, kumbusu au kumkumbatia
- kula pamoja
- kulala kitanda kimoja
- kuvaa nguo za muathiriwa au kufua nguo, taulo, malazi au choo, ukifuata maagizo uliyopewa
- kwa kumuuguza mtu aliye na virusi vya ukimwi au ugonjwa wa Ukimwi, ikiwa utafuata maagizo
- kuumwa na wadudu
Sources
- Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
- Audiopedia ID: sw011005