Ni nini ninachostahili kujua kuhusu maradhi kama kikohozi mafua na maradhi mengine makali zaidi
Kikohozi na mafua ni kawaida katika maisha ya watoto na siyo maradhi yanayo tishia maisha ya mtoto muhusika.
Lakini wakati mwingine, kikohozi ni alama ya maradhi mengine hatari kama vile pumu na kifua kikuu. Mtoto ambaye anapumua kwa kasi au kwa shida, anaweza akawa anaugua ugonjwa hatari wa pumu. Pumu ni maambukizi makali ya mapafu na yasipotibiwa kwa haraka, yaweza kusababisha kifo. Mtoto aliye na maambukizi haya ya pumu, anahitaji matibabu ya dharura kutoka wahudumu wa afya. Baadaye, mhudumu anaweza kutoa rufaa kwenye kituo kiingine cha afya.
Pumu ni maradhi yanayo ongoza zaidi katika kusababisha vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano ikifuatiwa kwa karibu na magonjwa ya kuharisha. Takribani watoto milioni mbili hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa pumu. Pumu inauwa watoto wengi kuliko magonjwa ya Ukimwi, Malaria na Surua pamoja. Moja kati ya vifo tano vya watoto chini ya umri wa miaka mitano husababishwa na magonjwa ya mapafu.